Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais wa kwanza wa Zambia Kaunda afariki dunia

KAUN DA WEEB Rais wa kwanza wa Zambia Kaunda afariki dunia

Thu, 17 Jun 2021 Chanzo: eatv.tv

Rais wa Kwanza wa Zambia, Kenneth Kaunda, amefariki dunia hii leo katika Hospitali ya Jeshi ya Maina Soko iliyopo Lusaka alipokuwa akipatiwa matibabu, akiwa na umri wa miaka 97.

Submitted by Agnes Kibona on Alhamisi , 17th Jun , 2021 Rais wa Kwanza wa Zambia, Kenneth Kaunda, wakati wa uhai wake

Vyanzo vya habari vimeeleza kuwa Muasisi huyo wa Taifa la Zambia, amefariki dunia akiwa anapatiwa matibabu kuanzia juma hili kutokana na maradhi ya muda mrefu yaliyokuwa yakimsumbua.

Kenneth Kaunda alitumikia taifa hilo la Zambia katika nafasi ya urais kuanzia mwaka 1964 hadi 1991.

Chanzo: eatv.tv