Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais wa Zimbabwe kuzindua rasmi bunge jipya

Mnangagwa 4 1.png Rais wa Zimbabwe kuzindua rasmi bunge jipya

Tue, 22 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa anatazamiwa leo, Novemba 22, anatarajiwa kufungua rasmi Bunge jipya lenye viti 650 jijini Harare ambalo limejengwa na China.

Kwa mujibu wa gazeti la serikali la Herald, Mnangagwa atatumia fursa hiyo kutoa hotuba yake kuhusu hali ya nchi hiyo.

Hotuba ya kiongozi huyo itafuatwa na ya Waziri wa Fedha ambaye atasoma bajeti ya kitaifa ya 2023, ripoti inasema kwamba ujenzi huo ulianza mwaka wa 2018, na kwamba usanifu huo unachanganya sifa za jadi za Zimbabwe na Kichina.

Hata hivyo, China ilifadhili mradi huo wa ujenzi wa Bunge la Kitaifa na Seneti kama zawadi kwa Zimbabwe na liko kilomita 18 kaskazini magharibi mwa mji mkuu wa Harare.

Kampuni ya Ujenzi ya Construction Group (SCG) iliyotekeleza mradi huo wa ujenzi uliofadhiliwa kikamilifu na serikali ya China, ilisema kuwa ni jengo la kihistoria na dhihirisho ya urafiki thabiti kati ya serikali ya China na Zimbabwe.

SCG ilikamilisha majengo hayo katika muda wa miezi 42, na kuchelewa kwa miezi 10 nyuma ya ratiba huku ucheleweshaji ukihusishwa na kuzuka kwa janga la Covid-19.

Haya yanajiri huku mataifa mengi barani Afrika yakiendelea kuzongwa na madeni na mikopo ya China. Zimbabwe, ambayo ina deni kubwa ya China, bado inategemea nchi hiyo ambayo iko tayari kutoa mikopo kwa Harare kutokana na rekodi yake mbaya ya ulipaji madeni.

Wakati wa enzi za utawala wa marehemu Robert Mugabe, Zimbabwe iliathirika vibaya uchumi kutokana na kutengwa na kuwekewa vikwazo na nchi za Magharibi kuhusiana na madai ya ukiukaji wa haki za binadamu na udanganyifu katika uchaguzi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live