Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais wa Zimbabwe awasili nchini kumuaga Hayati Rais Magufuli

6bb3257d311f21768f750f6feba39c01 Rais wa Zimbabwe awasili nchini kumuaga Hayati Rais Magufuli

Mon, 22 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

Rais wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa amekuwa wa kwanza kuwasili nchini kuhudhuria shughuli za kuuaga mwili wa Hayati, Rais Dk John Pombe Magufuli itakayofanyika kesho Uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.

Akizungumza na waandishi wa habari jioni hii katika uwanja huo, Msemaji wa Serikali, Dk Hassan Abbasi amesema marais wengine watakaohudhuria ni Uhuru Kenyatta Rais wa Kenya, Rais wa Malawi Lazarus Chakwera, Rais wa Comoro Azali Assoumani, Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi, na Rais wa Zambia Edgar Lungu.

Wengine ni Rais wa Namibia Hage Geingob, Rais Botswana Mokwaeetsi Masisi, Rais Afrika Kusini Cyril Ramaphosa, Rais wa DRC Felix Tshisekedi na viongozi watakowakilisha marais Waziri Mkuu wa Rwanda, Waziri wa Mambo ya Nje wa Angola na Makamu wa Rais wa Burundi.

"Mataifa ambayo marais watatuma wawakilishi wao ni Rwanda, Angola na Burundi na jumla ya Jumuiya 50 za Kimataifa na Kikanda zitatuma wawakilishi wao," amesema Dk Abbasi.

Aidha, amewakaribisha wananchi kukaa barabarani ili kumpungia na kumuaga kiongozi wao mara mwili utapowasili Jijini Dodoma leo na kesho asubuhi mara watapokuwa wanaelekea bungeni na kwenye uwanja wa Jamhuri huku akiwasisitiza kuendelee kumuombea dua Hayati Dk Magufuli.

"Nitoe wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kumuaga mpendwa wetu aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kesho hapa Dodoma katika uwanja wa Jamhuri,”ameongeza Dk Hassan Abbasi.

Chanzo: www.habarileo.co.tz