Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais wa Zimbabwe atilia mkazo mageuzi ili kuongeza ufanisi katika sekta ya umma

Mnangagwa 4 1.png Rais wa Zimbabwe atilia mkazo mageuzi ili kuongeza ufanisi katika sekta ya umma

Sun, 17 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe amesisitiza kuwa serikali yake itaendelea kutekeleza sera yake ya mageuzi ili kuimarisha ufanisi wa sekta ya umma nchini humo.

Mnangagwa amesema hayo wakati wa hafla ya kusainiwa mikataba ya utendajikazi wa mwaka wa fedha wa 2024 mbele ya mawaziri wa serikali, wakuu wa mashirika ya umma, serikali za mitaa na viongozi wengine wakuu wa serikali yake.

Amesema: "Serikali itaendelea kutekeleza jukumu muhimu la kuimarisha utekelezaji wa ajenda ya mageuzi katika sekta ya umma."

Ameongeza kwa kusema: “Serikali itaendelea na ajenda ya mageuzi hadi taasisi, mifumo na michakato yetu ya sekta ya umma itakapofikia ufanisi wa hali ya juu unaoendana na matakwa ya utoaji huduma na matarajio ya wananchi."

Amesema, licha ya mawaziri kadhaa wa serikali na viongozi wengine wakuu kupewa tunzo kutokana na utendaji wao wa kuridhisha mwaka jana, lakini utendaji jumla katika sekta ya umma hauridhishi na haujafikia viwango anavyotaka.

Ikumbukwe kuwa, Waziri wa Kilimo wa Zimbabwe, Anxious Masuka alitangazwa kuwa waziri wa serikali aliyefanya vizuri zaidi mwaka 2023 kwa mwaka wa pili mfululizo, huku Amon Murwira, Waziri wa Elimu ya Juu na Vyuo Vikuu, Ubunifu, Maendeleo ya Sayansi na Teknolojia wa nchi hiyo akishinda nafasi ya pili.

Nchi ya kusini mwa Afrika ya Zimbabwe inakabiliwa na changamoto nyingi za kijamii ikiwemo miripuko ya magonjwa mbalimbali kama mripuko wa kipindupindu wa mwaka jana ambao uliua makumi ya watu na kuambukiza maelfu ya wengine.

Hivi sasa serikali ya Harare imekuja na mikakati mbalimbalai ya kukabiliana kwa nguvu na changamoto kama hizo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live