Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais wa Zambia hajalipwa mshahara wake miezi 8 sasa

Hlichema Pre.jpeg Rais wa Zambia, Hakainde Hichilema

Wed, 6 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Zambia, Hakainde Hichilema mwenye umri wa miaka 59 amewashangaza wananchi wa taifa lake baada ya taarifa kuibuka kuwa hajachukua mshahara wake pamoja na marupurupu mbalimbali kwa takribani zaidi ya miezi nane.

Taarifa kutoka wizara inayohusika na malipo ya mshahara wa rais huyo, imedai kuwa Hakainde Hichilema ameamua kuacha fedha hizo kwa makusudi ili zilisaidie taifa lake.

Wakati wa kampeni za kugombea urais wa nchi hiyo Hichilema alidai kuwa mshahara haukuwa sehemu ya vipaumbele vyake vilivyomsukuma kugombea nafasi hiyo ya juu nchini Zambia.

“Suala la mshahara si suala la maana kwa sababu pesa haikuwa kivutio chetu cha kutufanya tugombanie urais na sio kwamba serikali haikuwa tayari kulipa, nia yangu na motisha ni kuona jinsi tunaweza kuboresha maisha ya watu.”

Rais Hichilema ni mtaalam wa masuala ya uchumi na pia ni mfanyabiashara mkubwa nchini Zambia akiwa na makampuni mbalimbali anayomiliki kabla ya kuingia madarakani, alifanikiwa kushinda Urais baada ya miaka 15 akiongoza chama cha upinzani na kumshinda rais aliyekuwa madarakani wakati huo Edgar Lungu kwa zaidi ya kura million moja.

Rais Hichilema pia amekuwa akiishi katika makazi yake binafsi yaliyopo New Kasama jijini Lusaka, kilomita nyingi kutoka Nkwazi House, ambapo ndipo makazi rasmi ya Rais wa Zambia yaliyopo ndani ya viwanja vya Ikulu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live