Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais wa Zambia awashangaza watu kuhudhuria Mkutano Mkuu UN kwa ndege ya abiria

Aikande 678 Rais wa Zambia, Hakainde Hichilema

Mon, 20 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Zambia Hakainde Hichilema ameondoka Lusaka kuelekea New York ambako atahudhuria mkutano wa 76 wa Baraza Kuu la UN ambapo amesafiri kwa ndege ya abiria badala ya ndege ya Rais huku akiwa na Wasaidizi wachache.

Wazambia wamepongeza hatua hiyo wakisema inalenga kubana matumizi hasa ukizingatia kuwa Hichilema alitangaza kuwa alipoingia madarakani hivi karibuni aliikuta Hazina ya Nchi hiyo ikiwa tupu bila pesa za kutosha kuendesha Nchi.

Mkutano huo wa 76, unatarajiwa kuhudhuriwa na wakuu wa nchi duniani na Kwa mara ya kwanza katika kipindi cha zaidi ya miaka sita, Rais wa Tanzania atakuwa mmoja wa washiriki katika mkutano huo

Chanzo: www.tanzaniaweb.live