Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais wa Zambia akataa kuishi IKulu

ZAMBIA2436 Rais mpya wa Zambia, Hakainde Hichilema, akataa kuishi Ikulu

Thu, 26 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais mpya wa Zambia Hakainde Hichilema amekataa kutoka kwenye makazi yake binafsi kwenda Ikulu, ripoti ya gazeti la Serikali la nchini Zambia, Daily Mail imeeleza.

Hatua hiyo imeelezwa wakati ambapo mtangulizi wake Edgar Lungu anatoka kwenye makazi ya Ikulu wiki hii.

Katibu Mkuu wa chama cha Hichilema, Batuke Imenda, amenukuliwa akisema kuwa kiongozi huyo mpya atafanya kazi ikulu, lakini ataendelea kuishi kwenye makazi yake binafsi, yaitwayo nyumba ya jamii.

''Kama alivyosema kabla ya kula kiapo, Rais wetu ataendelea kuishi kwenye nyumba yake huko New Kasama. Anajisikia vyema akiwa kwenye nyumba ya jamii. Unapolinganisha maeneo hayo mawili, nyumbani kwake ni bora,'' Bw. Imenda alisema kwa mujibu wa Zambia Daily Mail.

Tangazo hilo la kuwa Bw. Hichilema hataenda kuishi Ikulu limekuja baada ya Bw. Lungu, ambaye aliangushwa kwa zaidi ya kura milioni moja kwenye uchaguzi wa tarehe 12 mwezi Agosti, kuchapisha ujumbe kwenye ukurasa wa twitter akisema amekuwa ''kumbukumbu nzuri '' ya muda alioutumia ikulu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live