Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais wa Zambia akanusha kuunga mkono haki za wapenzi wa jinsia moja

Hakainde Hichilema.?fit=719%2C470&ssl=1 Rais wa Zambia Hakainde Hichilema

Tue, 31 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Zambia Hakainde Hichilema amesema serikali yake haihamasishi haki za wapenzi wa jinsia moja, tovuti ya Lusaka Times imeripoti, ikinukuu matamshi yake katika ibada ya kanisa.

Nchi hiyo ya kusini mwa Afrika ni moja ya nchi ambazo vitendo vya mapenzi ya jinsia moja ni kinyume cha sheria.

Rais anaripotiwa kuwaambia waumini kwamba msimamo wake kuhusu haki za wapenzi wa jinsia moja haujabadilika tangu akiwa upinzani.

Aliwataka Wazambia "kutozingatia mambo ambayo hayana umuhimu".

Katiba ya Zambia inaitambulisha nchi hiyo kuwa ya Kikristo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live