Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais wa Ukraine afanya mazungumzo na Rais wa Uganda

Rais Wa Ukraine Afanya Mazungumzo Na Rais Wa Uganda Rais wa Ukraine afanya mazungumzo na Rais wa Uganda

Thu, 23 Feb 2023 Chanzo: Bbc

Rais wa Uganda Yoweri Museveni na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky wamefanya mazungumzo kwa mara ya kwanza, kwa mujibu wa taarifa ya rais wa Ukraine.

Ujumbe waTweeter wa rais wa Ukraine ulisema alielezea mipango ya amani ya Ukraine katika Umoja wa Mataifa.

Alisema pia walijadili uwezekano wa maendeleo ya uhusiano baina ya nchi hizo mbili.

Bw Zelensky alisema kuwa alitarajia ushirikiano wa karibu hasa katika kuimarisha usalama wa chakula.

Mazungumzo hayo yamekuja wakati Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lenye wanachama 193 lilipokutana kujadili hoja iliyoungwa mkono na Ukraine ya kutaka kupigwa kura kuhusu azimio la kupatikana kwa amani nchini Ukraine.

Bunge limepigia kura maazimio matatu ya kupinga uvamizi wa Urusi katika mwaka uliopita, na kupokea kati ya kura 140 na 143 za ndio.

Kura ya hivi punde inakuja kabla tu ya maadhimisho ya miaka ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.

Chanzo: Bbc