Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais wa Tunisia amfuta kazi waziri mwingine ndani ya miezi 2

Tunisiaaaa Tunisia Rais Rais wa Tunisia amfuta kazi waziri mwingine ndani ya miezi 2

Thu, 23 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Kais Saied wa Tunisia leo Jumatano ameamua kumpiga kalamu na kusitisha majukumu ya Waziri wa Ajira na Mafunzo, Nasreddine Nsibi, hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa mapema leo na Ofisi ya Rais huyo wa Tunisia.

Huyu tayari ni waziri wa tatu aliyepigwa kalamu na kufutwa kazi na rais huyo wa Tunisia katika muda wa miezi miwili iliyopita. Taarifa hiyo haikueleza sababu ya kufukuzwa kazi.

Mbali na nafasi yake ya uwaziri wa masuala ya ajira, Nsibi alikukwa anashikilia pia wadhifa wa msemaji rasmi wa serikali ya Tunisia na haijulikani nafasi hiyo pia amepokwa au la.

Katika taarifa hiyo hiyo rais wa Tunisia amemteua Mounir Ben Rjiba kuwa waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo.

Tarehe 7 mwezi huu wa Februari, Rais Saied alimfuta kazi Waziri wa Mambo ya Nje Othman Jerandi, mwezi mmoja baada ya kumfukuza kazini Waziri wa Biashara Fadhila Rabhi.

Hali si shwari nchini Tunisia. Katikati ya mwezi huu wa Februari, askari usalama wa nchi hiyo waliwatia nguvuni wanaharakati wengine watatu wa kisiasa wa nchi hiyo.

Shirika la habari la IRIB liliripoti kuwa, vikosi vya usalama vya Tunisia vimewakamata Noureddine Al-Bahiri, Noureddine Boutar na Lazhar Al-Akrimi wanasheria na wanaharakati wa kisiasa wa nchi hiyo.

Taarifa hiyo ilisema pia kuwa, Rached Ghannouchi, kiongozi wa Vuguvugu la Ennahda la Tunisia, alitoa taarifa ya kulaani kukamatwa Nouruddin Al-Bahiri, mmoja wa wanachama waandamizi vuguvugu hilo na Nouruddin Butar, mkurugenzi wa kituo cha redio cha Mosaic FM.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live