RAIS wa Tunisia Kais Saeid amemfukuza kazi mkuu wa televisheni ya taifa, Mohamed Lissaad Dahech, na kumteua wa kushikilia nafasi hiyo kwa muda.
Awali, Saeid aliwafuta kazi maofisa wengi wa serikali. Alianza jukumu la uongozi mwishoni mwa juma baada ya kulisimamisha Bunge na kumuondoa Waziri Mkuu.
Wapinzani wa rais wamemshutumu kwa kupanga mapinduzi nchini humo.
Lakini anasisitiza kuwa ametekeleza wajibu wake ndani ya mamlaka yake wakati wa mzozo nchini humo.
Tunisia inakabiliwa na changamoto ya kuzorota kwa uchumi na kuongezeka kwa maambukizi ya Covid-19, na kusababisha kuongezeka kwa wasiwasi kimataifa.