Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais wa Somalia aishutumu Ethiopia

Rais Wa Somalia Rais wa Somalia aishutumu Ethiopia

Mon, 19 Feb 2024 Chanzo: Bbc

Rais wa Somalia Hassan Sheik Mohammed ameishutumu Ethiopia kwa "kuvunjia heshima" kwenye mkutano wa kilele wa Umoja wa Afrika (AU) unaoendelea mjini Addis Ababa akisema vikosi vya usalama vilijaribu kumzuia kufika eneo la mkutano huo.

Alisema baadaye aliruhusiwa kuingia.

Sheik Mohammed, ambaye alisafiri Addis Ababa kuhudhuria mkutano huo, amewaambia waandishi wa habari siku ya Jumamosi kwamba nchi yake imekatishwa tamaa na Ethiopia kutokana na "jaribio la kuhalalisha" makubaliano yasiyokuwa ya lazima yaliyotiwa saini na Eneo la Somaliland na Addis Ababa.

Makubaliano hayo yaliyotiwa wsaini Siku ya Mwaka Mpya yanasemekana kutoa nafasi kwa Ethiopia isiyo na bandari kupata ufikiaji wa kilomita 20 ya ukanda wa pwani na kusababisha mvutano wa kidiplomasia kati ya majirani hao wawili.

"Ethiopia inataka kunyakua ardhi ya Somalia", Bw. Shiek Mohammed alisema na kuongeza "hadi sasa kuna maafisa wakuu wa kijeshi huko Somaliland kuandaa mazingira" ya utekelezaji wa mpango huo.

Alisema Ethiopia inazidisha mzozo huo.

Mamlaka bado haijajibu madai ya hivi punde lakini Ethiopia ilikuwa imekanusha shmadai ya kutaka kunyakua madaraka.

Chanzo: Bbc