Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais wa Somalia aionya Ethiopia kuhusu mkataba wake na Somaliland

Rais Wa Somalia Aionya Ethiopia Rais wa Somalia aionya Ethiopia kuhusu mkataba wake na Somaliland

Wed, 24 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais Hassan Sheikh Mohamud wa Somalia ameionya Ethiopia na kuitaka isichukue hatua zozote za kutekeleza mkataba tata wa bandari iliowekeana na eneo lililojitenga la Somaliland.

Kwa mujibu wa makubaliano ya MOU yaliyotiwa saini Januari 1, 2024, Somaliland imeikodisha Ethiopia kilomita 20 za ufuo wake kuzunguka bandari ya Berbera, kwenye Ghuba ya Aden, kwa miaka 50 kwa madhumuni ya kijeshi na kibiashara. Ikumbukwe kuwa, Ethiopia ni nchi isiyo na bandari na ndoto yake kubwa ni kuwa na njia ya kuunganisha nchi hiyo na maji ya kimataifa.

Katika mahojiano aliyofanyiwa na televisheni ya Al Jazeera jana Jumanne, Rais Mohamud amesema kuwa, mali za Ethiopia zitalazimika kupita katika ardhi ya Somalia ili kufika eneo lililokodishwa na kuionya vikali Addis Ababa isijaribu kuchukua hatua kama hiyo.

Amesema: "Hadi sasa Waethiopia hawajakanyaga ardhi ya Somalia. Ikiwa watafanya hivyo, basi hilo litakuwa tatizo katika ngazi tofauti.”

Misri, ambayo inahusika katika mzozo tofauti na Ethiopia kuhusu bwawa kuu la Blue Nile, imeapa kusimama na Mogadishu katika mzozo wa Somaliland. Ahadi hizo za Misri zilitolewa hivi karibuni katika mazungumzo baina ya Rais Mohamud wa Somalia na mwenzake wa Misri, Jenerali Abdel Fattah el-Sisi.

Ethiopia inalenga kuanzisha kambi ya jeshi la wanamaji katika ardhi iliyokodishwa na Somaliland na kupata bandari kwa ajili ya mauzo na biashara zake za baharini kwenye Bahari Nyekundu na Mfereji wa Suez. Hatua hiyo inaweza kuirahisishia Ethiopia kuyafikia maeneo ya nje na ya kimataifa. Kwa sasa, Addis Ababa inaitegemea zaidi Djibouti kijinchi kidogo ambacho hakikidhi shughuli zake za bandari kwa biashara za ndani na nje.

Somaliland, eneo la Somalia ambalo lilijitenga na Somalia mwaka 1991 baada ya vita vya umwagaji damu, limekaribisha mpango huo wakati hasa kwa vile inatafuta kutambuliwa kimataifa na kuwa na fursa zaidi za kiuchumi za kuipiku Mogadishu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live