Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud amefanyiwa upasuaji wa bega katika Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), ofisi ya rais inasema.
Bw Mohamud anapata nafuu kutokana na upasuaji huo "mdogo",ofisi yake ilisema Alhamisi.Haikutoa maelezo zaidi juu ya kile kilichotokea kwenye bega lake.
Rais alikaa Abu Dhabi kwa siku chache, ambapo pia alikutana na maafisa wakuu wa Imarati, Shirika la Habari la Kitaifa la Somalia (Sonna) linaripoti.
Baadaye alisafiri hadi Riyadh, Saudi Arabia, kuhudhuria mkutano wa kilele wa Saudi-Afrika.
Tangu kuchaguliwa tena mwaka jana, Bw Mohamud amesafiri katika mataifa kadhaa, yakiwemo mataifa ya Ghuba, kutafuta uungwaji mkono kwa mashambulizi ya serikali yake dhidi ya al-Shabab.