Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais wa Somalia afanya mazungumzo ya usalama na kiongozi wa Eritrea

Rais Wa Somalia Afanya Mazungumzo Ya Usalama Na Kiongozi Wa Eritrea Rais wa Somalia afanya mazungumzo ya usalama na kiongozi wa Eritrea

Mon, 18 Mar 2024 Chanzo: Bbc

Rais wa Eritrea Isaias Afwerki na Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud wamefanya mazungumzo ya pande mbili katika mji mkuu wa Eritrea, Asmara.

Wakati wa mkutano "wa kina" siku ya Jumapili, viongozi hao wawili walijadili masuala ya kikanda, ikiwa ni pamoja na mapambano ya Somalia dhidi ya wanamgambo, Waziri wa Habari wa Eritrea Yemane Meskel alichapisha kwenye X.

Mazungumzo kuhusu "mada muhimu ya kikanda na kimataifa" pia yaliangaziwa katika mkutano wao, Shirika la Habari la Kitaifa la Somalia lilisema, bila kutoa maelezo zaidi.

Hii ilikuwa ni ziara ya pili ya Rais Mohamud nchini Eritrea mwaka huu na ya sita tangu aingie madarakani Mei 2022, akiangazia uhusiano mkubwa kati ya nchi hizo mbili.

Rais Mohamud alitembelea Asmara mara ya mwisho mwezi Januari huku kukiwa na mvutano na nchi jirani ya Ethiopia kuhusu makubaliano kati ya Addis Ababa na jamhuri iliyojitangaza ya Somaliland.

Mpango huo unapingwa na serikali ya Somalia. Video iliiochapishwa kwenye X inamuonyesha Rais Isaias na mgeni wake Mohamud wakitembea-tembea katika mitaa ya Asmara, huku wakazi wakishangilia na kupiga picha.

Eritrea imekuwa ikitoa mafunzo kwa maelfu ya wanajeshi wa Somalia ili kuongeza nguvu katika jeshi la Somalia huku wanajeshi wa Umoja wa Afrika wakitarajiwa kuondoka katika nchi hiyo ya Pembe ya Afrika mwishoni mwa mwaka huu. Article share tools

Chanzo: Bbc