Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais wa Sierra Leone ashusha tuhuma nzito kwa Marekani

Siera Leon.jpeg Rais wa Sierra Leone ashusha tuhuma nzito kwa Marekani

Sun, 17 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais Julius Maada Bio wa Sierra Leone aliituhumu Marekani Ijumaa kuwa ilimshinikiza kuingilia mchakato wa uchaguzi wa nchi hiyo uliofanyika June 24, kauli ambayo inapingana na msimamo ambao umekuwa ukionyeshwa na serikali ya Washington kuhusiana na kuwa huru uchaguzi wa nchi hiyo.

Rais huyo wa Sierra Leone amesema hayo katika mazungumzo yaliyofanyika katika chuo kimoja cha Marekani huko Washington na kuongeza kuwa matatizo yalizidi katika kilele cha kutangazwa matokea ya uchaguzi wa nchi hiyo ya Kiafrika. Wakati wa kutolewa mashinikizo hayo Tume ya Uchaguzi ya Sierra Leone ECSL ilikuwa imeshamaliza kuhesabu kura zote na kukamilisha michakato unaohusiana na suala hilo na nilitakiwa kusimamisha mchakato huo, hivyo sielewi nani anamtuhumu mwingine kuhusiana na uingiliaji katika uchaguzi huo. Amesema alikataa mashinikizo ya Marekani kuhusu jambo hilo kutokana na kuwa Tume ya Uchaguzi ya nchi hiyo ni huru na inajitegemea na wala sikuwa na wasiwasi wowote kuhusiana na kazi ya taasisi hiyo. Rais Bio mwenye umri wa miaka 59 alichaguliwa tena kuongoza nchi hiyo licha ya uchaguzi kuwa na utata na uliokosolewa na wapinzani na wachunguzi wa kimataifa. Katika taarifa ya pamoja wakaguzi kutoka Marekani, Umoja wa Ulaya, Ufaransa, Ireland na Ujerumani walisema wao pia kama vile wakaguzi wa ndani, walikuwa na wasiwasi juu ya kukosekana uwazi katika mchakato wa majumuisho ya kura nchini humo.

Uchaguzi nchini Sierra Leone Kabla ya uchaguzi huo, baadhi walidhani kupanda kwa bei ya vyakula na hali mbaya ya kiuchumi ingeupa upinzani fursa, lakini Rais Bio alishinda kwa asilimia 56.17. Bio ameongeza Washington ilikuwa inaitisha kufanya mapinduzi kwa kisingizio cha kutilia shaka uhuru wa uchaguzi nchini humo. Wakaguzi wa Marekani walidai kuwa walitaka kufanyike duru ya pili ya uchaguzi ili kuthibitisha suala hilo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live