Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais wa Senegal asema ataondoka madarakani tarehe 2 mwezi Aprili

Rais Wa Senegal Asema Ataondoka Madarakani Tarehe 2 Mwezi Aprili Rais wa Senegal asema ataondoka madarakani tarehe 2 mwezi Aprili

Fri, 23 Feb 2024 Chanzo: Bbc

Rais wa Senegal Macky Sall amesema ataondoka madarakani tarehe 2 Aprili wakati muhula wake utakapokamilika, lakini bado haijafahamika ni lini uchaguzi utafanyika ili kumchagua mrithi wake.

Alisema tarehe ya uchaguzi itategemea mdahalo wa kitaifa uliopangwa kuanza Jumatatu, ambao unajumuisha mashirika ya kiraia, vyama vya kisiasa na wagombea.

"Tarehe 2 Aprili 2024 dhamira yangu kama mkuu wa Senegal inafikia kikomo...ningependa mjadala huu utatuliwe kwa uwazi," alisema wakati wa mahojiano ya televisheni.

Tangazo lake linapunguza hofu kwamba alikuwa akipanga kuongeza muda wake, huku kukiwa na mzozo wa kisiasa.

Bw Sall amekuwa chini ya shinikizo la kutangaza tarehe ya uchaguzi tangu kujaribu kuuchelewesha mapema mwezi huu.

Alikuwa akitaka kuahirisha uchaguzi hadi Desemba ili mizozo kuhusu kustahiki kwa wagombea wengine iweze kutatuliwa.

Lakini mahakama kuu ya nchi hiyo ilisema kucheleweshwa huko ni kinyume cha katiba, na kutaka uchaguzi ufanyike "haraka iwezekanavyo".

Senegal iko hatarini baada ya uchaguzi kucheleweshwa

Chanzo: Bbc