Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais wa Senegal apendekeza mswada wa msamaha kumaliza mzozo wa kisiasa

Rais Wa Senegal Apendekeza Mswada Wa Msamaha Kumaliza Mzozo Wa Kisiasa Rais wa Senegal apendekeza mswada wa msamaha kumaliza mzozo wa kisiasa

Tue, 27 Feb 2024 Chanzo: Bbc

Rais wa Senegal, Macky Sall amependekeza msamaha kwa wale waliopatikana na hatia kuhusiana na maandamano ya kisiasa katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita.

Alisema hili litawezesha "kutuliza joto la kisiasa na kuimarisha zaidi uwiano wetu wa kitaifa".

Alisema hayo katika mazungumzo ambayo kwa kiasi kikubwa yamesusiwa na upinzani na makundi ya kiraia.

Rais huyo anayekabiliwa na mzozo amekosolewa vikali kwa kuahirisha uchaguzi uliokuwa ufanyike Jumapili, bila kuweka tarehe mpya.

Mahakama ya Katiba imeamua kwamba uchaguzi huo ufanyike haraka iwezekanavyo.

Mswada wa msamaha uliopendekezwa - ambao Bw Sall anasema utawasilishwa bungeni Jumatano - tayari umepingwa na wapinzani wake.

Wanasema lengo ni kuhakikisha kuwa wanajeshi wa vikosi vya usalama na Rais Sall mwenyewe hawawezi kufunguliwa mashtaka kwa mauaji ya waandamanaji.

Chanzo: Bbc