Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais wa Rwanda awafuta kazi zaidi ya wanajeshi 200

Rais Wa Rwanda Awafuta Kazi Zaidi Ya Wanajeshi 200.png Rais wa Rwanda awafuta kazi zaidi ya wanajeshi 200

Fri, 30 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Rwanda Paul Kagame amewafuta kazi takriban wanajeshi 214 wakiwemo maafisa kadhaa wakuu wa kijeshi.

Taarifa fupi ya Wizara ya Ulinzi ya Rwanda, iliyowekwa kwenye ukurasa wake rasmi wa X asubuhi ya leo, ilisema kuwa maafisa waliofutwa kazi ni pamoja na Meja Jenerali Martin Nzaramba na Kanali Dkt Etienne Uwimana.

"Pia ameidhinisha kufutwa na kubatilishwa kwa maafisa 195 wa vyeo vingine vya Jeshi la Ulinzi la Rwanda," ilisema taarifa hiyo.

Hakuna sababu iliyotolewa kwa hatua hiyo, lakini ilitangazwa saa chache baada ya Kagame kukutana na maafisa wakuu wa kijeshi, akiwemo Mkuu wa Majeshi Jenerali Mubarakh Muganga.

Tovuti inayounga mkono serikali ya New Times, iliripoti kwamba Kagame na maafisa wa kijeshi walijadili vipaumbele vya amani na usalama vya Rwanda.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live