Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais wa Nigeria na Makamu wake wapatiwa chanjo ya Corona

2d3dfe91 Beea 4caf B79b 6e4087c0c58a 660x400.jpeg Rais wa Nigeria na Makamu wake wapatiwa chanjo ya Corona

Mon, 8 Mar 2021 Chanzo: millardayo.com

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari na Makamu wake Yemi Osibanjo wamekuwa watu wa kwanza kupatiwa chanjo ikiwa ni njia ya kuwahakikishia wananchi kuwa chanjo ndiyo kinga muafaka dhidi ya virusi vya corona.

Nigeria wiki iliyopita ilipokea chanjo ya Covid 19 ikiwa ni mwanzoni mwa awamu ya pili ya mapambano dhidi ya janga la virusi vya corona, huku kampeni ikiendelea kuelimisha raia kuhusu Covid na hatua za msingi za kuchukuliwa kuzuia na maambukizi.

Rais Buhari na Makamu wake Osinbajo walikuwa wa kwanza kwenye orodha ya viongozi wa siasa Nigeria kupatiwa chanjo kama njia moja ya kushawishi wananchi kuchukua chanjo hiyo ambayo ni mahsusi kwa ajili ya kujikinga na janga la Covid.

Mara baada ya kupatiwa chanjo Rais Buhari alitumia fursa kuwaomba raia wa nchi hiyo kufahamu vizuri umuhimu wa kupatiwa chanjo ili kujikinga na virusi vya corona kama yeye alivyofaya pamoja na makamu wake.

Mwenyekiti wa Kamati ya Rais juu ya Covid 19, Boss Mustapha amesema hatua ya rais na makamu wake kupatiwa chanjo inaonyesha dhahiri kuwa uongozi wa Nigeria una imani kwa chanjo zilizoagizwa kutoka nje na kwamba hazina madhara.

EXCLUSIVE: MAAJABU YA MTOTO GENIUS WA HESABU, “SIJAFUNDISHWA, WAKUBWA HAWANIWEZI”

Chanzo: millardayo.com