Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais wa Nigeria asepa Uingereza kuchunguza afya

Buhari Nigeria Rais wa Nigeria aelekea Uingereza kuchunguza afya

Wed, 2 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari ameondoka kwenda Uingereza kwa ajili ya uchunguzi wa kawaida wa kimatibabu.

Kwa mujibu wa  mshauri wake maalum Femi Adesina alisema kupitia  taarifa kwenye Twitter.Rais huyo anatarajiwa kurejea Nigeria wiki ya pili ya mwezi huu,

Bw Buhari mwenye umri wa miaka 79, amekuwa akitafuta matibabu mara kwa mara nje ya nchi tangu alipoingia madarakani mwaka 2015.

Mara nyingi amekuwa akikosolewa kwa kutafuta matibabu nje ya nchi huku mfumo wa huduma za afya nchini Nigeria ukikabiliwa na usimamizi mbaya na ufadhili mdogo.

Muda wake kama rais kwa mihula miwili mfululizo unafikia kikomo mwezi Februari wakati nchi hiyo itakapofanya uchaguzi mkuu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live