Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais wa Nigeria achukua hatua kukabiliana na kupanda kwa gharama

Rais Wa Nigeria Achukua Hatua Kukabiliana Na Kupanda Kwa Gharama Rais wa Nigeria achukua hatua kukabiliana na kupanda kwa gharama

Tue, 1 Aug 2023 Chanzo: Voa

Rais wa Nigeria Jumatatu alitangaza hatua kadhaa za kukabiliana na kupanda kwa gharama ya maisha, ikiwemo kutoa tani laki mbili za nafaka ya akiba baada ya ghala la chakula kuporwa kaskazini mashariki mwa nchi.

Tangu alipoingia madarakani mwezi Mei, Rais Bola Tinubu amechukua maamuzi kadhaa yanayokusudia kuimarisha uwekezaji wa muda mrefu, lakini hatua hizo zimeathiri vibaya kaya na kuongeza umaskini katika taifa hilo lenye uchumi mkubwa na idadi kubwa ya watu barani Afrika.

Mwezi uliopita, rais huyo aliondoa ruzuku ya mafuta, na kusababisha bei ya petroli kuongezeka maradufu na kupanda kwa bei ya chakula.

“Uchumi wetu unapitia hali ngumu na inawaathiri. Gharama ya mafuta imepanda. Chakula na bei nyingine zimepanda pia,” Tinubu alisema katika taarifa kwenye televisheni Jumatatu.

Katika kile alichokiita mbinu za kuwapunguzia mzigo wananchi, aliahidi dola milioni 264 kwa kilimo, dola milioni 165 kwa biashara za viwango vya kati na ndogo, na dola milioni 99 kwa viwanda.

Chanzo: Voa