Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais wa Nigeria aagiza maafisa wa usalama kuokoa wanafunzi waliotekwa nyara

Rais Wa Nigeria Aagiza Maafisa Wa Usalama Kuokoa Wanafunzi Waliotekwa Nyara Rais wa Nigeria aagiza maafisa wa usalama kuokoa wanafunzi waliotekwa nyara

Thu, 14 Mar 2024 Chanzo: Voa

Rais wa Nigeria aliamuru maafisa wa usalama kutolipa fidia kwa ajili ya kuachiliwa kwa zaidi ya wanafunzi 250 wa shule ya msingi waliotekwa nyara na watu wenye silaha wiki iliyopita, waziri wa habari alisema Jumatano.

Ndugu wa wanafunzi hao wanasema watekaji nyara wameomba fidia kubwa ili kuwaachilia wanafunzi waliotekwa nyara shuleni mwao Alhamisi iliyopita katika kijiji cha Kuriga kaskazini magharibi mwa jimbo la Kaduna.

Magenge ya wahalifu mara nyingi huteka nyara watu wengi kaskazini mwa Nigeria, yakilenga shule, vijiji na barabara kuu.

Katika miaka mitatu iliyopita, mamia ya wanafunzi walitekwa nyara. Waathirika wa utekaji nyara nchini Nigeria mara nyingi huachiwa huru baada ya mazungumzo na mamlaka, ingawa maafisa wanakanusha malipo ya fidia kufanyika.

Kwa kuzingatia msimamo rasmi wa serikali, waziri Mohammed Idris alisema Rais Bola Tinubu aliwaambia maafisa wa usalama wanaowatafuta wanafunzi kuhakikisha “hakuna hata senti moja inayolipwa”.

“Rais ameviagiza vyombo vya usalama kwamba kwa sababu ni suala la dharura lazima vihakikishe watoto hawa na wale wote waliotekwa nyara wanarejeshwa nyumbani wakiwa salama,” aliwambia waandishi wa habari kufuatia mkutano wa baraza la mawaziri katika mji mkuu Abuja.

Chanzo: Voa