Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais wa Namibia kupatiwa matibabu ya saratani Marekani

Rais Wa Namibia Kupatiwa Matibabu Ya Saratani Marekani Rais wa Namibia kupatiwa matibabu ya saratani Marekani

Thu, 25 Jan 2024 Chanzo: Voa

Rais wa Namibia Hage Geingob alitarajiwa kuwasili Marekani Jumatano kwa ajili ya kufanyiwa matibabu ya saratani, ofisi ya rais imetangaza.

Uchunguzi wa mara kwa mara wa kimatibabu mapema mwezi huu, ulifichua kwamba Geingob mwenye umri wa miaka 82 alikuwa anaugua saratani, ofisi yake ilisema wiki iliyopita, bila kutoa maelezo kuhusu hali yake.

Rais amekubali ombi la wanasayansi na wataalamu wa matibabu mjini Los Angeles, California, kufanyiwa matibabu mapya ili kukabiliana na seli za saratani, ilisema taarifa ya rais Jumatano, na kuongeza kwamba kwamba atakuwa Marekani kwa wiki moja kabla ya kurejea Namibia kwendelea na matibabu.

Makamu wa rais Nangolo Mumba, atakaimu kama rais wakati Geingob akiwa nje ya nchi.

Wasiwasi kuhusu hali ya afaya ya kiongozi huyo umekuwa ukiongezeka, huku ripoti zikieleza kwamba alikiri mwaka jana, kuwa afya yake ilikuwa imedhoofika. Geingob anatarajiwa kustaafu baadaye mwaka huu, baada ya kuhudumu kwa mihumla miwili kama rais.

Chanzo: Voa