Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais wa Namibia Hage Geingob azikwa mjini Windhoek

Rais Wa Namibia Hage Geingob Azikwa Mjini Windhoek Rais wa Namibia Hage Geingob azikwa mjini Windhoek

Sun, 25 Feb 2024 Chanzo: Bbc

Rais wa Namibia Hage Geingob aliyefariki mapema mwezi huu amezikwa katika mji mkuu Windhoek.

Waziri mkuu wa kwanza wa Namibia na rais wa tatu alifariki akiwa na umri wa miaka 82 baada ya kuugua saratani kwa muda mfupi.

Geingob alizikwa kwa heshima kamili ya kijeshi katika sehemu maalum ya kaburi la mashujaa

Mazishi yake yalihudhuriwa na wakuu wa nchi na serikali na viongozi wa kigeni akiwemo Binti Mfalme Anne.

Maelfu ya wananchi wa Namibia wakipeperusha bendera ya taifa na waliovalia nguo nyeusi walijiunga na viongozi wa kigeni kutoka mataifa kadhaa.

Bw Geingob ambaye alikuwa mwanachama mwanzilishi wa Namibia kupata uhuru,alisaidia kuunda katiba mpya.

Chanzo: Bbc