Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais wa Msumbiji ashitakiwa UK deni la Tsh trilioni 4.61

Nyusi Pic Filipe Nyusi , Rais wa Msumbiji

Fri, 29 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi anashtakiwa mjini London na kampuni ya Abu Dhabi kwa kushindwa kulipa kiasi cha dola bilioni 2 na trilioni4.61 za kitanzani jambo ambalo limesababisha kuporomoka kwa uchumi wa taifa hilo.

Kampuni hiyo ambayo inamilikiwa na bilionea wa kifaransa Iskandar Safa, iliingia makubaliano na kampuni za Serikali ya Msumbiji ya kusambaza samaki aina ya Tuna pamoja na meli za usalama baharini.

Ili kuwezesha mkakati huo Serikali nchi humo ilichukua mkopo wa siri mwaka 2013 na 2014 wenye asilimia takribani 12 katika pato la taifa na fedha hizo zinatajwa kutumika kinyume na malengo yaliyowekwa jambo ambalo limepelekea kushindwa kulipa madeni hayo katika muda muafaka.

Taarifa ya Kampuni hiyo inaeleza kuwa makubaliano hayo yalifanyika wakati Rais Nyusi akiwa hajaingia madarakani japo anahusika moja kwa moja katika kesi hiyo na kusema kuwa fedha hizo alizitumia kufanya kampeni zake za urais.

Tayari Kampuni hiyo imewasilisha barua ya Mahakamani katika Ofisi ya Rais huyo iliyopo jijini Maputo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live