Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais wa Misri athibitisha kuwa atawania muhula wa tatu

Rais Wa Misri Athibitisha Kuwa Atawania Muhula Wa Tatu Rais wa Misri athibitisha kuwa atawania muhula wa tatu

Tue, 3 Oct 2023 Chanzo: Bbc

Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi amethibitisha kuwa atawania muhula wa tatu katika uchaguzi uliopangwa kufanyika mwezi Disemba.

Mkuu huyo wa zamani wa jeshi amekuwa madarakani tangu aliposaidia kumuondoa madarakani Mohammed Morsi, kiongozi wa Muslim Brotherhood mwaka 2013.

Wanaharakati wanasema muhula wake madarakani umeangaziwa na ukandamizaji wa kikatili wa upinzani na kuporomoka kwa uchumi wa Misri.

Katiba ilibadilishwa miaka minne iliyopita ili kurefusha muda wake madarakani na majaribio ya wapinzani kuandaa azma ya kuaminika ya kugombea urais yanaripotiwa kutatizwa na urasimu wa Misri.

Chanzo: Bbc