Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

'Rais wa Misri amesimamia msako dhidi ya wapinzani'

'Rais Wa Misri Amesimamia Msako Dhidi Ya Wapinzani' 'Rais wa Misri amesimamia msako dhidi ya wapinzani'

Mon, 2 Oct 2023 Chanzo: Bbc

Makundi ya kutetea haki za binadamu yanasema kwamba matumizi ya mateso na mamlaka ya Misri yameenea sana na yana utaratibu kiasi cha kuwa uhalifu dhidi ya ubinadamu.

Katika ripoti iliyowasilishwa kwa Kamati ya Umoja wa Mataifa dhidi ya Mateso, makundi sita yalizungumzia kupigwa, shoti za umeme, unyanyasaji wa kingono na kunyimwa huduma za matibabu na wanachama wa huduma za usalama.

Walisema mateso yametumika kama zana ya kisiasa kupunguza upinzani.

Mwenyekiti mpya wa Kamati ya Mahusiano ya Kigeni ya Seneti ya Marekani, Ben Cardin, ametishia kuzuia msaada wa kijeshi wa Marekani kwa Misri ikiwa Cairo haitachukua hatua madhubuti kuboresha rekodi yake kuhusu haki za binadamu.

Wakati wa utawala wake wa muongo mmoja, Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi amesimamia ukandamizaji dhidi ya wapinzani.

Chanzo: Bbc