Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais wa Misri aagiza maafisa wa serikali kuhamia kwenye mji mpya kupunguza foleni mjini

Egypt New Town Rais wa Misri aagiza maafisa wa serikali kuhamia kwenye mji mpya

Wed, 3 Nov 2021 Chanzo: BBC

Rais wa Misri Abdul Fattah al-Sisi ameelekeza mamlaka za Serikali kuanza kuhamia kwenye mji mpya wa kiserikali kuanzia mwezi ujao.

Msemaji wa Rais Sisi alisema hatua hiyo itakuwa seheu ya majaribio ya miezi sita ya kuhamia makao mapya.

Makao mapya ya kiutawala ya serikali yalianza yamejengwa kilometa 45 mashariki mwa jiji la Cairo.

Mpango huo uliotumia mabilioni ya dola unalenga kwa mujibu wa maofisa umefanywa ili kuepuka msongamano katika jiji la Cairo, ambapo mji huo unaweza kuchukua watu zaidi ya milioni 6.

Pamoja na mji huo wa kiserikali utakaokuwa na maofisi ya kiserikali, pia eneo hilo litakuwa na makazi ya balozi mbalimbali pamoja na makazi ya Rais.

Chanzo: BBC