Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais wa Mauritania anaisihi Mali kujiunga tena na kikosi cha Afrika

Rais Wa Mauritania Anaisihi Mali Kujiunga Tena Na Kikosi Cha Afrika Rais wa Mauritania anaisihi Mali kujiunga tena na kikosi cha Afrika

Tue, 11 Jul 2023 Chanzo: Voa

Mali ilitangaza uamuzi wake hapo Mei 2022 ikishutumu kupoteza uhuru na kujiimarisha ndani ya kikundi cha kikanda. Mwaka 2021, Chad ilikusudiwa kukabidhi urais wa G5 kwa Mali lakini haikufanya hivyo hatua ambayo Bamako iliitafsiri kama uingiliaji kati wa Ufaransa

Rais wa Mauritania siku ya Jumatatu aliisihi Mali kujiunga tena na kikosi cha Afrika Magharibi kinachopambana dhidi ya wanajihadi na kundi la kikanda linalojulikana kama G5 Sahel ambalo lilijiondoa mwaka jana.

Mali ilitangaza uamuzi wake hapo Mei 2022 ikishutumu kupoteza uhuru na kujiimarisha ndani ya kikundi cha kikanda. Mwaka 2021, Chad ilikusudiwa kukabidhi urais wa G5 kwa Mali lakini haikufanya hivyo hatua ambayo Bamako iliitafsiri kama uingiliaji kati wa Ufaransa.

Natumai uondokaji huu utakuwa wa mfupi sana, Rais Mohamed Ould Cheikh El Ghazouani alisema katika hotuba katika mji mkuu wa Nouakchott. Alisema uamuzi wa utawala wa kijeshi, Ufaransa kuondoa vikosi vyake vya mwisho kutoka Mali vilivyopelekwa chini ya kikosi chake cha kupambana na jihadi cha Barkhane, pamoja na mgogoro wa Sudan ni matukio ya kusikitisha.

Chanzo: Voa