Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais wa Mali akamatwa kwa kufanyia baraza la mawaziri mabadiliko

25e349bb323a892c Rais wa Mali akamatwa kwa kufanyia baraza la mawaziri mabadiliko

Tue, 25 May 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Hali ya wasiwasi imekumba Mali baada ya kundi la wanajeshi kumkamata na kumzuia kaimu rais Bah Ndaw na waziri mkuu Moctar Quane kufuatia mabadiliko tata katika Baraza la Mawaziri.

Kulingana na shirika la habari la kimataifa, waziri wa ulinzi Souleymane Doucoure pia alikamatwa pamoja na wawili hao.

Wanajeshi waliwapeleka watatu hao katika kambi ya jeshi ya Kati nje ya jiji kuu la taifa hilo Bamako, saa chache baada ya wanajeshi wawili kupoteza nyadhifa zao katika baraza la mawaziri.

Mnamo Jumanne, Agosti 19, 2020, wanajeshi walivamia Bamako na kumkamata Rais Ibrahim Boubacar Keita pamoja na maafisa wengine wakuu serikalini.

TUKO.co.ke inatambua kuwa kukamatwa kwa watatu hao ni kufuatia mabadiliko yaliyofanyiwa baraza la mawaziri ambapo wanachama wawili wa junta waliopindua serikali ya Mali 2020 waliondolewa.

Katika taarifa, Jumuiya ya Kiuchumi ya Mataifa ya Afrika Magharibi (ECOWAS) iliyosema inaunga mkono utawala wa Mali kurejeshwa mikononi mwa raia, Umoja wa Afrika (AU), Umoja wa Mataifa na Maafisa wa Marekani ni miongoni mwa mashirika ambayo yalishtumu mapinduzi hayo.

Hali hii ya sasa huenda ikazua vita katika taifa hilo la Magharibi mwa Afrika ambapo makundi ya kigaidi ya Kiislamu ambayo yanahusishwa na al Qaeda na Islamic State yanatawala sehemu kubwa ya Mali.

Msukosuko wa kisiasa na vita vya wanajeshi vimeathiri juhudi za mataifa ya kigeni na majirani kukomboa taifa hilo na hivyo kuchangia vita eneo hilo.

Mnamo Agosti 2020, Rais Uhuru Kenyatta alijiunga na viongozi wengine kuhimiza taifa hilo kufuata katiba baada ya Keita kuzuiliwa katika kambi ya wanajeshi ya Kati.

Katika taarifa, Uhuru alihimiza Mali kutafuta suluhu ya haraka itakayorejesha amani na kuzingatia demokrasia.

READ ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke