Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais wa Malawi mgeni rasmi 'Mashujaa Day'

Kwenda Kenya Rais wa Malawi, Lazarus Chakwera

Mon, 18 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Malawi, Lazarus Chakera anatarajiwa kuwasili nchini Kenya Oktoba 19,2021.

Rais huyo ambaye ataongozana na mke wake Monica, atakuwa nchini humo kwa ziara maalum ya kikazi ya siku tatu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ikulu ya Kenya, inaeleza kuwa Rais huyo atakuwa mgeni rasmi katika sherehe za Mashujaa zinazotarajiwa kufanyika tarehe 20 Oktoba, 2021.

Aidha baada ya hapo watapokekelewa na Rais Kenyatta pamoja na mke wake Margaret Kenyatta siku ya Alhamisi Oktoba 21, 2021.

Rais Chakwera awali alikuwa ni mhubiri wa kanisa la kiinjilisti kabla ya kuchaguliwa kuongoza taifa hilo mwezi Juni 2020 dhidi ya mshindani wake Peter Mutharika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live