Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais wa Liberia apunguza mshahara wake

Joseph Boakai Ds Rais wa Liberia apunguza mshahara wake

Thu, 11 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Liberia, Joseph Boakai ametangaza kuwa atapunguza mshahara wake kwa 40% ikiwa ni sehemu ya kuweka mfano wa utawala unaowajibika na kuonesha mshikamano na Wananchi wa Nchi hiyo.

Mishahara ya Serikali imekuwa ikichunguzwa vikali hivi karibuni huku Walaiberia wakilalamikia kupanda kwa gharama ya maisha ambapo Mtu mmoja kati ya watano anaishi chini ya $2 (Tsh.5,309) kwa siku katika Nchi hiyo ya Afrika magharibi.

Rais huyo mwezi February alinukuliwa akisema mshahara wake wa mwezi ni $13,400 (Tsh.35,571,479) na hivyo upungufu huo utapunguza hadi $8,000 (Tsh.21,236,704) ambapo hatua ya Boakai inalingana na ile ya Mtangulizi wake, George Weah, ambaye alipunguza 25% ya mshahara wake.

Baadhi ya Watu katika Taifa hilo wamepongeza uamuzi wa Boakai lakini wengine wanashangaa ikiwa ni kujitolea kweli kweli kutokana na kwamba anapokea marupurupu kama vile posho ya kila siku na bima ya matibabu.

Bajeti ya ofisi ya Rais huyo ni karibu $3m (Tsh.bilioni 7,941,210,000 ) mwaka huu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live