Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais wa Kenya aondoa marufuku ya miaka sita ya ukataji miti

Rais Wa Kenya Aondoa Marufuku Ya Miaka Sita Ya Ukataji Miti Rais wa Kenya aondoa marufuku ya miaka sita ya ukataji miti

Mon, 3 Jul 2023 Chanzo: Bbc

Rais wa Kenya William Ruto ameondoa marufuku ya ukataji miti iliyowekwa miaka sita iliyopita.

Rais alisema hatua hiyo "imechelewa" akitaja haja ya kubuni nafasi za kazi na kufungua sekta za uchumi zinazotegemea mazao ya misitu.

Wasiwasi juu ya athari za ukataji miti kwenye mazingira na mabadiliko ya tabia nchi ulisababisha kupigwa marufuku kwa ukataji miti mwaka wa 2018.

Lakini akizungumza Jumapili mjini Molo eneo la Bonde la Ufa, Bw Ruto alitetea kuondolewa kwa marufuku hiyo akisema kusitishwa kwa ukataji miti kumekuwa "upumbavu".

"Miti inaoza msituni huku watu wakihangaika kupata mbao, unaona upumbavu huo?"Aliuliza.

Alisema serikali ilitoza ushuru kwa yeyote anayeagiza mbao na samani kutoka nje katika bajeti ya hivi majuzi "kwa sababu tunataka yote hayo yafanywe na watu wa Kenya".

Marufuku ya ukataji miti imeathiri baadhi ya maeneo ambayo watu wengi walitegemea ukataji miti kama chanzo cha maisha yao.

Kuondolewa kwa marufuku hiyo kunakuja wakati serikali ikiendelea na mpango wake wa kupanda miti bilioni 15 katika kipindi cha miaka 10 ili kuongeza miti

Chanzo: Bbc