Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais wa Ghana asema Burkina Faso inashirikiana na kundi la Wagner

Rais Wa Ghana Asema Burkina Faso Inashirikiana Na Kundi La Wagner Rais wa Ghana asema Burkina Faso inashirikiana na kundi la Wagner

Fri, 16 Dec 2022 Chanzo: Bbc

Rais wa Ghana Nana Akufo-Addo amesema serikali ya Jamhuri jirani ya Burkina Faso imeanza kushirikiana na mamluki wa Urusi kutoka Kundi la Wagner.

Kauli hii ilitolewa na Rais wa Ghana katika mkutano wa pamoja na waandishi wa habari na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Anthony Blinken.

"Leo, mamluki wa Urusi wako kwenye mpaka wetu wa kaskazini. Burkina Faso, ikifuata Mali, iliingia makubaliano ya kuajiri vikosi vya Wagner," alisema.

"Kulingana na taarifa yangu, mgodi ulioko kusini mwa Burkina uligawiwa kwao kama malipo. Waziri Mkuu wa Burkina Faso alikuwa Moscow kwa siku 10. Ukweli kwamba wanafanya kazi kwenye mpaka wetu wa kaskazini ni shida sana kwetu," alisema.

Ghana ililaani vikali uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine.

Hata hivyo, serikali ya Burkina Faso bado haijatoa maoni yoyote kuhusu habari hii.

Mwakilishi wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Ufaransa, Anne-Clair Legendre, akijibu swali la mwandishi wa habari alisema: “Msimamo wetu kuhusu Wagner unajulikana. Wanamgambo wa Wagner wamejipambanua hasa nchini Msumbiji, Jamhuri ya Afrika ya Kati na Mali. Ni wazi kwamba jambo hili linajulikana kwa mamlaka ya Burkina Faso."

Mtandao rasmi wa Telegramu cha muundaji wa "kikundi cha Wagner" Yevgeny Prigozhin kilitoa jibu la ombi kutoka chombo cha habari cha Reuters kutokana na taarifa ya rais wa Ghana:

"Sasa, kuhusu Wagner. Wagner itajijua yenyewe ni wapi litakapokuwa au kutokuwa. Jambo moja ninaloweza kusema kwa uhakika ni kwamba Wagner haiendelezi migodi, haichimbi dhahabu na haishiriki katika miradi mingine ya kiuchumi."

Chanzo: Bbc