Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais wa Ethiopia aahidi ushirikiano wa kiuchumi na Tanzania

D67b5f11f7344ba7a2f5f287010e6c34 Rais wa Ethiopia aahidi ushirikiano wa kiuchumi na Tanzania

Tue, 26 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

Rais wa Ethiopia, Salhe-Work Zewde amesema nchi yake ipo tayari kuongeza ushirikiano wa kufanya biashara na Tanzania kwa lengo kukuza uchumi baina ya nchi hizo mbili upate kukuwa.

Zewde amesema hayo leo akiwa wilayani Chato mkoani Geita wakati wa ziara yake ya siku moja hapa nchini ambapo alipokelewa na mwenyeji wake rais wa Dk John Magufuli.

“Mimi na Rais Magufuli tumekubaliana mambo mapya kwenye mahusiano katika maeneo ya biashara na uwekezaji kwakuwa wote tunaamini kwamba waafrika wnatakiwa kuwekeza katika nchi za kiafrika” amesema Zewde.

Aidha, Zewde amesema mahusiano baina ya nchi hizi bili yanatakiwa yawe na mizizi imara ndio maana itakapofika mwezi wa Machi au Aprili mwaka huu kitafanyika kikao cha Tume ya Ushirikiano ‘Joint Commission’ kitakachopitia makubaliano ya mikataba yote iliyofanyika ikiwemo kuangalia maeneo mapya ya ushirikiano.

Rais wa Tanzania Dk John Magufuli amesema kuwa ushirikiano uliopo baina ya nchi hizi mbili umewezesha bodi ya utalii hapa nchini kuingia makubaliano ya kuweka matangazo ya vivutio vya utalii katika shirika la ndege la nchi hiyo hiyo jambo lililosaidia kuongeza idadi ya watalii wanaokuja hapa nchini.

Chanzo: habarileo.co.tz