Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais wa Colombia aahidi kuinua meli yenye mamilioni ya dhahabu na fedha

Rais Wa Colombia Aahidi Kuinua Meli Yenye Mamilioni Ya Dhahabu Na Fedha Rais wa Colombia aahidi kuinua meli yenye mamilioni ya dhahabu na fedha

Tue, 7 Nov 2023 Chanzo: Bbc

Rais wa Colombia, Gustavo Petro, amewaambia mawaziri wa serikali kuharakisha juhudi za kuondoa tani mia mbili za dhahabu, fedha na zumaridi kutoka kwa meli ya Uhispania iliyozama katika visiwa vya Caribbean miaka mia tatu iliyopita.

Meli hiyo kwa jina la San José galleon ilizamishwa na wanajeshi wa Uingereza katika mji wa bandari wa Cartegena mwaka wa 1708, wakati taifa la Colombia lilikuwa himaya ya Uhispania.

Meli hiyo imetajwa kuwa ya thamani zaidi kati ya meli zilizozama, kwa sababu ilikuwa imebeba hazina ya thamani zaidi iliyowahi kupotea baharini.

Scott Williams, ambaye ni rais wa jumuiya ya wanahistoria wa baharini, na ambaye amewahi kuhusika na shughuli za kutafuta meli zilizozamishwa, ameiambia BBC kwa nini meli hiyo inaaminika kubeba mali yenye dhamani kubwa.

‘’Watu wanaotafuta hazina iliyopotea watakuambia, wao wanafahamu kuwa meli hiyo inathamani kubwa zaidi. Ninaona vigumu kuamini kwamba ina thamani ya dola bilioni ishirini au zaidi kwa sababu hiyo ni hazina nyingi sana. Lakini nadhani kivutio cha fedha nyingi kiasi hicho pamoja na dhahabu, fedha na zumaridi ndio inachowapa moyo zaidi.’’

Meli hiyo ilikuwa, inarejea Uhispania na shehena yenye dhamani kubwaili kufadhili vita, vita vya mfululizo vya Uhispania.

Ilikuwa inatoka Bolivia na ilikuwa imebeba sarafu za dhahabu zinazokaridiriwa kuwa mamilioni ya dola pamoja na fedha na zamaradi kutoka migodi ya Amerika Kusini, na pengine vito vya sanaa.

Juhudi za kujaribu kurejesha meli hiyo hadi juu ya bahari huenda ikawa kibarua kigumu sana.

Eneo linakisiwa meli hiyo imezama ina urefu wa mita mia sita.

Kwa hivyo kujaribu kuinua meli hiyo, itakuwa kazi ngumu sana na kujaribu kuopoa vito vya sanaa kutoka kwa meli hiyo haitakuwa kazi ngumu sana lakini kumbuka kwa urefu wa kiasi hicho baharini sio kazi rahisi.

Rais Petro amehaidi kuwa atahakikisha kuwa shehena hiyo ya thamani imepatikana kabla ya kumalizika kwa muhala wake, miaka mitatu ijayo.

Serikali ya Uhispania imedai kuwa shehena hiyo ni mali yake, ikisema kuwa meli ya San Jose, ilikuwa meli ya jeshi lake la wanamaji wakati ilipozamishwa.

Chanzo: Bbc