Gaborone, Botswana. Rais wa Botswana, Mokgweetsi Masisi ametangaza kujitenga kwa muda wa siku 14 kutokana na hofu ya kuambukizwa virusi vya corona.
Uamuzi wa Rais Masisi umeanza rasmi Jumamosi iliyopita.
Taarifa iliyotolewa na ofisi ya Rais ilisema kuwa uamuzi huo unafuatia safari ya kiongozi huyo nchini Namibia.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Rais Masisi aliongozana na maofisa wa nchi hiyo kwenda Namibia kuhudhuria mkutano uliokuwa ukijadili hatua muhimu zilizochukuliwa katika kudhibiti virusi vya corona (covid-19).
“Rais Masisi atakuwa akifanya kazi katika makazi yake rasmi,” ilisema taarifa hiyo.
Hata hivyo, taarifa hiyo ilisema kuwa katika kipindi chote kiongozi huyo pia atakuwa mbali na familia yake.
Pia Soma
- Watu 23 wafariki dunia kwa jaribio la kutoroka gerezani kisa corona
- ATCL yasitisha safari zote za ndege nje ya Tanzania
- Luis atoboa siri tishio la namba linavyompasua kichwa Simba
Naye Kansela wa Ujerumani, Angela Markel amejiweka karantini nyumbani kwake akihofia kuwa ameambukizwa corona.
Kansela Merkel ametangaza kujiweka karantini mwishoni mwa wiki baada ya kukutana na daktari aliyeambukizwa corona. Taarifa ya Wizara ya Afya ya Ujerumani ilisema kwa sasa Kansela Merkel anaendelea vizuri akisubiri majibu ya vipimo.
Hadi kufikia jana idadi ya waliombukizwa virusi vya corona nchini humo imefikia watu 22,672.