Rais wa Angola, Joao Lourenco siku ya Jumatatu amefanya mazungumzo na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky kwa njia ya simu ili kujadili vita inayoendelea baina yao na Urusi.
“Vita inayoendelea kati yao na Urusi ambayo inahusisha majeshi ya nchi hizo ni moja ya mada tulizojadiliana.” alisema Lourenco.
Aidha Rais wa Ukraine kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter ameandika kuwa moja ya mazungumzo yake na Rais wa Angola ni kuona namna ya kushirikiana ndani ya Jumuiya ya Umoja wa Mataifa.
Kwa mara nyingi Zelensky amekuwa akifanya mazungumzo na viongozi wa Afrika akiwa na lengo la kutaka kuungwa mkono juu ya mgogoro wake dhidi ya Urusi.
Angola imekuwa ni moja ya nchi nyingi za Afrika ambazo zimegoma kuunga mkono upande wowote ule katika vita hiyo kati ya Ukraine na Urusi