Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais wa Afrika Kusini: Putin hatahudhuria mkutano wa BRICS

Rais Wa Afrika Kusini: Putin Hatahudhuria Mkutano Wa BRICS Rais wa Afrika Kusini: Putin hatahudhuria mkutano wa BRICS

Wed, 19 Jul 2023 Chanzo: Bbc

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amethibitisha kuwa Rais wa Urusi Vladimir Putin hatahudhuria mkutano wa kilele wa BRICS utakaofanyika mjini Johannesburg mwezi ujao.

Hii inafuatia changamoto za kisheria za chama cha upinzani cha Democratic Alliance na Amnesty International ambacho kilidai kuwa kama nchi iliyosaini Mkataba wa Roma, Afrika Kusini inalazimika kumkamata kiongozi huyo wa Urusi ikiwa atakanyaga nchini Afrika Kusini.

Mwandishi wa BBC aliyeko mjini Johannesburg, Nomsa Maseko anasema, Serikali ya Afrika Kusini imesema makubaliano ya pamoja yamefikiwa kwamba Rais wa Urusi Vladimir Putin hatahudhuria mkutano wa kilele wa BRICS. Nchi hiyo sasa itawakilishwa na waziri wake wa mambo ya nje Sergey Lavrov.

Mkutano huo utahudhuriwa na viongozi wa Brazil, India, China na Afrika Kusini.

Hii inamaliza changamoto za kisheria na maumivu makubwa ya kichwa kwa Rais Cyril Ramaphosa baada ya kuwa chini ya shinikizo la kumkamata kiongozi wa Urusi ikiwa atahudhuria mkutano huo.

Shirika la Amnesty International lilijiunga na kesi iliyowasilishwa na chama cha upinzani cha Democratic Alliance ambacho kiliitaka Afrika Kusini kumkamata Putin na kumkabidhi kwa ICC ili akabiliwe na mashtaka ya uhalifu wa kivita.

Rais Ramaphosa alikuwa ameomba ruhusa kutoka ICC kutomkamata Putin akidai kuwa kufanya hivyo ni sawa na kutangaza vita dhidi ya Moscow, wakati Urusi mara kwa mara imeelezea waranti ya kukamatwa kwa ICC kuwa ni ya kuchukiza na batili kisheria kwa sababu nchi hiyo sio mwanachama wa mahakama hiyo.

Chanzo: Bbc