Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais mtarajiwa wa Senegal aahidi kukabiliana na ufisadi

Rais Mtarajiwa Wa Senegal Aahidi Kukabiliana Na Ufisadi Rais mtarajiwa wa Senegal aahidi kukabiliana na ufisadi

Tue, 26 Mar 2024 Chanzo: Bbc

Rais mtarajiwa wa Senegal, Diomaye Faye amesema atapambana na rushwa katika ngazi zote na kushiriki katika maridhiano ya kitaifa ili kuunganisha nchi hiyo.

Pia alidokeza kuwa nchi yake itasalia kuwa mshirika wa kimataifa wa kutegemewa na uhusiano wa kunufaishana.

Mgombea wa upinzani ambaye anatarajiwa kuthibitishwa kuwa rais ajaye wa Senegal anasema wapiga kura wamechagua kuachana na siku za nyuma.

Bassirou Diomaye Faye alikuwa akizungumza katika mkutano uliofurika wanahabari mjini Dakar – ikiwa ni wake wa kwanza tangu kuibuka na kura nyingi katika duru ya kwanza ya uchaguzi wa Jumapili.

Alisema atatawala kwa unyenyekevu na atakabiliana na ufisadi.

Bw Faye, ambaye ana umri wa miaka arobaini na nne, atakuwa mkuu wa taifa mwenye umri mdogo zaidi nchini Senegal.

Mapema mwezi huu bado alikuwa gerezani kwa mashtaka yakiwemo ya uasi.

Matokeo rasmi bado hayajatangazwa, lakini mgombeaji wa muungano unaotawala, Amadou Ba, amekiri kushindwa.

Rais anayeondoka, Macky Sall, alielezea ushindi wa Bw Faye kama ushindi kwa watu wa Senegal

Chanzo: Bbc