Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais mstaafu afikishwa kortini kwa uhaini

Rais 21 Rais mstaafu afikishwa kortini kwa uhaini

Thu, 4 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa zamani wa Sierra Leone, Ernest Bai Koroma amefikishwa mbele ya Mahakama kujibu mashtaka ya uhaini akidaiwa kujihusisha na jaribio la mapinduzi mwishoni mwa Novemba 2023.

Koroma aliyekuwa Rais kati ya 2007 na 2018, alihojiwa na Polisi mara tatu kabla ya kufunguliwa mashtaka ya mashambulizi ya silaha katika kambi ya jeshi na Gereza, jijini Freetown.

Katika shambulizi hilo, inadaiwa Wafungwa 2,000 walitoroka, miongoni mwao wakiwa ni watuhumiwa waliohusishwa na mapinduzi hayo.

Hata hivyo, tayari zaidi ya watu 50 wamekamatwa wakihusishwa na mashambulizi hayo, ikiwa ni pamoja na binti wa Mstaafu Koroma.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live