Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais mstaafu Niger atunukiwa tuzo ya Mo Ibrahim

D51d2e437cdd2c8a5b806115763d8c5e Rais mstaafu Niger atunukiwa tuzo ya Mo Ibrahim

Wed, 10 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

RAIS mstaafu wa Niger, Mahamadou Issoufou, ametunukiwa Tuzo ya Mo Ibrahim ya Ufanisi katika Uongozi kwa Afrika kwa mwaka 2020.

Taasisi ya Mo Ibrahim ilimtangaza mshindi huyo jana baada ya kukamilika kwa kikao cha Kamati Huru ya Tuzo.

Rais Issoufou alihudumu katika nafasi ya urais wa Niger kwa mihula miwili ya miaka mitano mitano kuanzia mwaka 2011 hadi 2020 na amekuwa kiongozi wa sita kupokea tuzo hiyo inayotambua ubora wa uongozi Afrika.

Lengo la tuzo hiyo ya Mo Ibrahim ni kuwatambua viongozi waliofanya mambo ya kipekee wakati walipokuwa madarakani ikiwemo kuziendeleza nchi zao, kuimarisha demokrasia na kulinda utawala wa sheria kwa faida ya watu wao.

Kamati ya tuzo hiyo ilimpongeza Rais Issoufou kwa uongozi uliotukuka baada ya kuichukua nchi hiyo ikiwa katika uchumi duni huku ikikabiliwa na changamoto lukuki.

Kamati hiyo ilisema wakati wote wa uongozi wake, alifanikiwa kukuza uchumi, alishiriki kuhakikisha kuna utulivu wa kikanda, kikatiba na kupigania demokrasia Afrika.

Wakati akitangaza tuzo hiyo jana, Mwenyekiti wa Kamati hiyo ambaye ni Rais mstaafu wa Botswana, Festus Mogae alisema “Katika nyakati ngumu za kisiasa na kiuchumi pamoja na msimamo mkali wa vurugu na kuongezeka kwa jangwa, Rais Mahamadou Issoufou aliwaongoza watu wake katika njia ya maendeleo.”

Alisema idadi ya wananchi wa Niger wanaoishi chini ya mstari wa umaskini imeshuka kutoka asilimia 48 hadi kufikia asilimia 40 katika muongo mmoja uliopita, hivyo kamati iliona Rais Issoufou amekidhi vigezo vya kuwa mshindi

Chanzo: www.habarileo.co.tz