Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais mpya wa Namibia aapishwa

Rais Mpya Wa Namibia Aapishwa Rais mpya wa Namibia aapishwa

Sun, 4 Feb 2024 Chanzo: Bbc

Rais Mpya wa Namibia Nangolo Mbumba ameapishwa kuwa rais wa nne wa Namibia baada ya rais Hage Geingob kufariki hospitalini mapema Jumapili.

Mbumba ambaye aliwahi kuwa makamu wa rais chini ya Geingob alikula kiapo chake cha ofisi katika ikulu ya nchi hiyo.

Netumbo Nandi_Ndaitwah alikula kiapo cha kuwa makamu wa rais mara moja.

Katika hali ya utulivu baada ya hafla hiyo, Mbumba alitoa pongezi kwa mtangulizi wake akimtaja kuwa mbunifu mkuu wa katiba na usanifu wa utawala wa Namibia.

Geingob alikuwa mwanachama mwanzilishi wa nchi ya kisasa baada ya ukoloni. Mbumba ataongoza nchi kwenye uchaguzi utakaofanyika baada ya muda wa miezi 9.

Chanzo: Bbc