Rais mpya wa Nigeria, Bola Tinubu amefanya mabadiliko makubwa kwenye vikosi vya Ulinzi na kuwalazimisha Wakuu wa Usalama na Wakuu wa Polisi kuondoka ikiwa chini ya mwezi mmoja baada ya kushika madaraka.
Tinubu ambaye aliapishwa Mei 29, ameweka usalama kuwa moja ya vipaumbele vyake vikuu na kuahidi mageuzi ya sekta hiyo, ikiwa ni pamoja na kuajiri askari zaidi na maafisa wa Polisi huku akiwalipa na kuwapa vifaa bora.
Hata hivyo, utaratibu huo sio kawaida kwa rais mpya wa Nigeria kuwataka wakuu wa usalama kustaafu mapema baada ya kuchukua madaraka, ambapo hivi karibuni pia alimchagua aliyekuwa Afisa Mkuu wa zamani wa Polisi, Nuhu Ribadu kama Mshauri wake wa Usalama wa Kitaifa.
Jeshi nchini Nigeria, linaendelea kupambana na waasi wa Kiislamu kaskazini-mashariki mwa nchi hiyo ujambazi na utekaji nyara kwa lengo la kulipia fidia kaskazini magharibi huku ukosefu wa usalama ukienea katika maeneo mengi ya nchi.