Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais avunja Bunge baada ya jaribio la mapindizu Guinea-Bissau

Guinea Bissauuu.jpeg Rais avunja Bunge baada ya jaribio la mapindizu Guinea-Bissau

Tue, 5 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Guinea-Bissau, Umaro Sissoco Embalo, jana Jumatatu aliamua kulivunja Bunge linalotawaliwa na upinzani, siku tatu baada ya mapigano ya silaha ambayo ameyataja kama "jaribio la mapinduzi" na ambayo yameitumbukiza nchi hiyo ndogo ya Afrika Magharibi katika mgogoro mwingine.

Taarifa iliyotolewa na Rais wa Guinea kwenye vyombo vya habari imesema: "Tarehe ya uchaguzi ujao wa Bunge itaainishwa wakati mwafaka kwa mujibu wa masharti ya Katiba."

Taarifa hiyo imeongeza kuwa: "Baada ya jaribio hilo la mapinduzi lililoongozwa na kikosi cha Gadi ya Taifa na kutokana na ushahidi mkubwa wa kuwepo njama ya kisiasa, utendaji wa kawaida wa taasisi za Jamhuri hauwezekani. Mambo haya yanathibitisha kuwepo kwa mgogoro mkubwa wa kisiasa."

Guinea-Bissau inasumbuliwa na misukosuko ya kisiasa na imekumbwa na msururu wa mapinduzi tangu ilipopata uhuru kutoka kwa Ureno mwaka 1974; na mara ya mwisho ilikuwa Februari mwaka jana 2022.

Viongozi wa Gadi ya Taifa walivamia majengo ya polisi wa mahakama siku ya Alhamisi iliyopita na kuwachukua Waziri wa Uchumi na Fedha, na Katibu wa Hazina ya Umma, Antonio Monteiro kwa ajili ya kuhojiwa. Baadaye waliingia katika kambi ya kijeshi katika mji mkuu Bissau, na kuanzisha mapigano ya silaha hadi Ijumaa asubuhi. Mapigano hayo yamesababisha vifo vya watu wasiopungua wawili.

Rais wa Guinea-Bissau, Umaro Sissoco Embalo ameonya kwamba machafuko hayo yatakuwa na "matokeo mabaya" .

Chanzo: www.tanzaniaweb.live