Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais ataka changamoto za kitaasisi zishughulikiwe

56117539 6.jpeg Rais ataka changamoto za kitaasisi zishughulikiwe

Thu, 27 Oct 2022 Chanzo: dar24.com

Rais wa zamani wa Niger, Mahamadou Issoufou, amesisitiza juu ya umuhimu wa ujenzi wa Mataifa katika mchakato wa kutuliza matukio ya mapinduzi barani Afrika na kusema upo umuhimu wa kuangalia changamoto za msingi za kitaasisi.

Issoufou ameyasema hayo mara baada ya kumalizika kwa Kongamano la kimataifa kuhusu amani na usalama barani Afrika, la jijini Dakar nchini Senegal, wakati ukanda wa Afrika Magharibi ukiwa na mivutano ya kisiasa, inayotokana na wimbi la mapinduzi ya kijeshi ya hivi karibuni.

Amesema, Jumuiya ya kimataifa zinapaswa kuzisaidia nchi za ukanda wa Sahel, huku akisisitiza mchango wa mataifa ya Magharibi, katika kulivuruga eneo hilo kwa uingiliaji wao wa kijeshi nchini Libya mwaka 2011.

Washiriki wa kongamano hilo, wanasema hali inayojiri katika ukanda huo, haimaanishi kuwa Waafrika wanaipa kisogo demokrasia, bali zipo sababu zinazopelekea kutokea kwa matukio mengi ya aina hiyo.

Chanzo: dar24.com