Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais apiga marufuku watumishi kwenda likizo nje ya nchi

Jenerali Brice Oligui Nguema Rais apiga marufuku watumishi kwenda likizo nje ya nchi

Wed, 21 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Mpito, Jenerali Oligui Nguema amepiga marufuku Maafisa wa Serikali wa nchi hiyo kusafiri nje ya nchi kwaajili ya likizo.

Pia, ameweka ukomo wa likizo kwa muda usiozidi wiki moja kwa Maafisa hao wa Serikali.

Msemaji wa Serikali ya Mpito alifafanua kuwa maamuzi haya yanalenga kuhamasisha Viongozi kuwa karibu na Wananchi huku akisisitiza kuwa ruhusa maalumu za kusafiri nje ya Nchi zitatolewa kwasababu za kiafya.

Aidha, maamuzi haya yanadaiwa kufanywa na Rais Nguema kama maandalizi ya kugombea Urais katika Uchaguzi ujao wa mwaka 2025.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live