Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais aliyekaa madarakani kwa muda mrefu zaidi duniani agombea tena

Nguema Rais aliyekaa madarakani kwa muda mrefu zaidi duniani agombea tena

Sun, 20 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais aliyekaa madarakani kwa muda mrefu zaidi duniani anawania kuchaguliwa tena ili kuendeleza utawala wake wa miaka 43 nchini Equatorial Guinea.

Rais Teodoro Obiang Nguema Mbasogo, 80, ameongoza serikali inayodaiwa kukiuka haki za binadamu ikiwa ni pamoja na kuteswa na kutoweka kwa watu.Baadhi ya wagombea wa upinzani wamejitokeza, lakini hawatarajiwi kushinda.

Rais huyu ameweka mizizi mikubwa kwa taifa hilo lenye utajiri mkubwa wa mafuta, huku wanafamilia yake wakiwa katika nafasi muhimu katika serikali.

Mwanawe wa kipekee, ambaye anahudumu kama Makamu wa Rais wa nchi hiyo, Teodoro "Teodorin" Nguema Obiang Mangue, amekuwa akifurahia maisha ya kifahari nchini Marekani na Ulaya, na hata anamiliki glovu za bei ghali zilizofunikwa na kioo ambazo hapo awali zilimilikiwa na Michael Jackson, kwa mujibu wa mamlaka ya Uingereza.

"Uchaguzi huo ni wa mapambo tu", Profesa Ana Lúcia Sá aliambia BBC."Hakuna kitakachobadilika," Profesa Sá, ambaye ni mtaalamu wa siasa na tawala za kimabavu za Kiafrika katika Taasisi ya Chuo Kikuu cha Lisbon, alisema, akiongeza kuwa "ana uhakika Obiang atachaguliwa kwa zaidi ya 95%" ya kura.

Hisia hii pia inaungwa mkono na mwanaharakati Tutu Alicante, ambaye aliliambia shirika la habari la Reuters: "Siku ya Jumapili watu watapiga kura ambayo serikali inawatarajia, kwa sababu huwezi kusema kwa uhuru mawazo yako nchini Equatorial Guinea."

"Upinzani haupati nafasi," Bw Alicante aliendelea. "Atafanya chochote kinachohitajika ili asiondoke madarakani."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live