Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais aliyehudumu kwa muda mrefu zaidi aanza muhula wa sita

D909429c 77cc 4c36 8425 1667b6691006 Rais aliyehudumu kwa muda mrefu zaidi aanza muhula wa sita

Fri, 9 Dec 2022 Chanzo: Bbc

Mkuu wa nchi aliyehudumu kwa muda mrefu zaidi duniani- Rais wa Equatorial Guinea, ameapishwa kuongeza nchi hiyo tena kwa muhula wa sita madarakani.

Teodoro Obiang Nguema Mbasogo, ambaye ana umri wa miaka 80, alikula kiapo chake kabla ya kukagua gwaride la jeshi.

Alitangaza kuwa- na wakati wote atakuwa – kiongozi wa watu wote wa Equatorial Guinea.

Alinyakua madaraka kwa mara ya kwanza katika mapinduzi ya mwaka 1979.

Wakosoaji wake wanasema tangu wakati huo uchaguzi umekuwa ukitawaliwa na wizi wa kura, huku upinzani ukizuiwa kushiriki na vyombo vya habari hudhibitiwa na serikali na washirika wake.

Chanzo: Bbc